Friday, June 20, 2014

Mashabiki Kenya wapigwa marufuku kutazama kombe la dunia Bar


SERIKALI ya Kenya imewataka watu kutazama mechi za kombe la dunia wakiwa majumbani kwao badala ya kwenda kwenye sehemu zenye mkusanyiko wa watu na sehemu za wazi ambazo si salama.

Onyo hilo linakuja baada ya shambulio la mapema wiki hii huko Pwani ya nchi hiyo ambalo liliacha watu wapatao 60 kupoteza maisha.

Tukio hilo lilifanyika huko Mpeketoni wakati watu wakitazama kombe la dunia.
Waziri wa mambo ya ndani amesema ingawa usalama umeimarishwa nchini humo lakini wamiliki wa Bar na Hotel wanatakiwa kuchukua tahadhari.

Kikundi cha kiislam cha Al-Shabab tayari kimetangaza kuhusika na tukio hilo la huko Mpeketoni ikiwa ni kulipa kisasi cha kuwepo kwa askari wa Kenya huko Somalia na kudai kuua waislam.

Lakini Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema mitandao ya kisiasa nchini Kenya inapaswa kubeba lawama .

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.