Paul Pogba ametoa kali baada ya kunaswa na camera akicheza game ya soka akiichezea Chelsea na kuonesha yuko njiani kuelekea kwenye timu hiyo.
Pogba anayeichezea Juventus alipigwa picha hiyo kwenye ndege akiwa na kikosi cha Ufaransa kwenye kombe la dunia ambapo alichagua kuichezea Chelsea na kujipanga kikosini kuonesha nia yake ya kujiunga na The Blues.
Pogba, 21, kwenye kikosi hicho cha Chelsea pia alimpanga mchezaji mwenzake wa Juventus Kevin Asamoah upande wa beki wa kushoto na mchezaji wa Real Madrid Jese akamuweka sehemu ya ushambuliaji katika mtazamo mpya wa Chelsea.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.