Saturday, June 14, 2014
Baada ya Spain kupigwa mkono Casillas ajitwika zigo la lawama
Golikipa wa Spain Iker Casillas amejibebesha zigo la lawama wakati mabingwa watetezi walipoanza vibaya kwa kichapo cha mabao 5-1 mbele ya Uholanzi.
Hispania chini ya kocha Vicente Del Bosque walitangulia kutumbukia wavuni lakini wakashindwa kuendeleza furaha yao na wakajikuta wakishindwa kuhimili presha ya Uholanzi waliorudi na kuwachakaza kwa kipigo kimono.
Casillas anakiri kuwa hakuwa kwenye kiwango kinachotakiwa kwenye mchezo huo na anakubali kulaumiwa.
Anasema hakufanya kama alivyotakiwa kufanya,tena katika mchezo kama ule wa ufunguzi kombe la dunia na hilo kwake anaona ni moja kati ya michezo ambayo sio bora kwake.
Hispania walitangulia kwa bao la Xabi Alonso kabla ya Uholanzi kurudisha kupitia kwa Robin van Persie aliyetupia mawili na akifunga moja ya mabao bora.
Mabao mengine ya Uholanzi yalitupiwa wavuni na Arjen Robben aliyefunga mawili na Stefan de Vrij.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.