Thursday, June 19, 2014

Mganga aendelea kumkaanga Ronaldo


Kauli ya mganga wa kienyeji wa Ghana,Nana Kwaku Bonsam kwamba yeye ndio anamroga mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ili asicheze mchezo wa kombe la dunia dhidi ya Ghana yanaendelea kutimia taratibu baada ya hapo jana mshambuliaji huyo kushindwa kuendelea na mazoezi na kutoka nje huku akiwa amefungwa barafu.

Kuumia kwake kunaleta mashaka ya kuweza kucheza katika michezo iliyobakia ya hatua ya makundi.
Itakumbukwa mganga huyo wa kienyeji wa Ghana alisema kuwa mshambuliaji huyo atakuwa anaumia na hakutakuwa na dawa yoyote itakayomuwezesha kupona kwakuwa yeye ndio anamroga.

Mganga huyo anasema alilazimika kutafuta mbwa wane walionona ili kuitengeneza dawa hiyo kali ya kumuumiza Ronaldo.
 
 
 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.