Wednesday, July 23, 2014

Mourinho atangaza utawala EPL


Kocha Jose Mourinho amesema anataka kuutawala msimu mpya na kuweka mipango ya utawala kwa muda wa muongo mmoja.

Boss huyo wa Chelsea na kikosi chake leo wanashuka dimbani katika maandalizi ya kabla ya msimu kucheza na RZ Pellets huko Klagenfurt, Austria.

Wachezaji waliosajiliwa wakati wa dirisha la usajili linaloendelea Diego Costa, Cesc Fabregas na Filipe Luis tayari wamejiunga na timu hiyo.

Mourinho amesema kama hatafikiri kuwa watashinda taji la EPL ni vyema akarudi nyumbani na kumuacha kocha mwingine kuchukua mikoba hiyo.

Anasema msimu uliopita waliishia nusu fainali ya Champions League ilikuwa ni kipindi cha mpito.

Anaongeza kuwa timu hiyo imekuwa timu ya ushindani kwa miaka 10 ikipitia katika hatua mbalimbali.

Van Gaal aponda ratiba ya Man U Pre-Seasson


Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal ameipinga ratiba ya klabu hiyo ya maandalizi ya kabla ya msimu huko Marekani.

United wanacheza dhidi ya Los Angeles Galaxy leo huko Pasadena kabla ya kupiga mechi nyingine huko Denver, Washington na Detroit.
Van Gaal, 62, amesema ratiba hiyo imekaa kibiashara zadi na haina msaada kwa maandalizi ya kikosi.

Anasema wanalazimika kusafiri umbali mrefu jambo ambalo halina matokeo bora sana.

Saturday July 26: Roma, Sports Authority Field, Denver - International Champions Cup
Wednesday July 30: Inter Milan, Fedex Field, Washington - International Champions Cup
Saturday August 2: Real Madrid, Michigan Stadium, Detroit - International Champions Cup

Mzozo wa Ukraine waikimbiza Shaktar Donetsk


Shakhtar Donetsk watacheza mechi zake za nyumbani huko Magharibi katika mji wa Lviv uliopo zaidi ya maili 600 kwasababu ya mgogoro uliopo Ukraine.

Wachezaji sita wa kigeni wamegoma kurudi huko Donetsk wakihofia mzozo huo.

Wachezaji waliogoma kurudi baada ya mechi yao ya kirafiki huko Lyon ni wachezaji watano raia wa Brazil na mmoja kutoka Argentina ambao ni Alex Teixeira, Fred, Dentinho, Douglas Costa, Facundo Ferreyra na Ismaily.
Kikosi hicho sasa kitakuwa kina fanya mazoezi yake huko Kiev na kusafiri kwenda kucheza mechi zake za champions league na mechi za ligi huko Lviv.

Mapigano yanaendelea katika baadhi ya maeneo huko Donetsk.

Rais wa klabu hiyo Rinat Akhmetov amesema wachezaji hao wanautumia mgogoro huo kutaka kuhama na kwenda kucheza timu nyingine.

Shakhtar hapo jana wameifunga Dynamo Kiev 2-0 huko Lviv,katika mchezo wa ufunguzi wa msimu.