Friday, February 28, 2014

West Brom yamtia kitanzini Anelka,yamtoa kikosini,kisa ishara ya kinazi


West Bromwich Albion imemsimamisha mshambuliaji wake Nicolas Anelka baada ya kufungiwa mechi 5 na kupigwa faini ya paundi elfu 80 kutokana na kushangilia kwa ishara ya kinazi.

Anelka, 34, alikataa kutumia ishara isiyoruhusiwa katika mchezo ambao timu yake ya West Brom ilitoka sare na West Ham December 8.

West Brom wamemsimamisha mpaka hapo baada ya matokeo ya rufaa na mapitio ya klabu kwakuwa Anelka anafikiria kukata rufaa juu ya hukumu hiyo ya FA.
Mfaransa huyo na timu yake ya sharia wametetea ishara hiyo ya ushangiliaji ambapo amesema ilikuwa ni katika kumuunga mkono rafiki yake mchekeshaji wa Ufaransa Dieudonne M'bala M'bala.

Ishara hiyo ya ushangiliaji ambayo aliionesha alipofunga bao la tatu na kufanya mchezo kuwa sare ya mabao 3-3 ilielezewa na Waziri mkuu wa Ufaransa Valerie Fourneyron kuwa ni mbaya na ya kushtua.

Jambo hilo pia liliwafanya wadhamini Zoopla,kutangaza kujitoa kuidhamini timu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.