Monday, February 10, 2014

Man U kimeo


Bao la dakika za mwisho la Darren Bent limemfanya kocha wa Fulham Rene Meulensteen kuondoka na pointi muhimu huko Old Trafford na kuendeleza msimu mbaya kwa Manchester United.

Steve Sidwell ndio alianza kuifungia Fulham bao la kuongoza kabla ya Robin van Persie kusawazisha na Michael Carrick kuifungia bao la pili United lakini akitokea benchi Bent akaisawazishia Fulham.

Huo ni muendelezo wa matokeo mabovu kwa United katika msimu huu ikiwa chini ya kocha Davis Moyes.





No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.