Akisimama urefu wake ni futi 5 na inch 8 lakini Eden Hazard amejipambanua kama mlaji bora kwenye timu ya taifa ya Belgium.
Chef wa timu ya taifa ya Belgium Wim Casteleyn amesema licha ya wachezaji wenzake kama Romelu Lukaku na Christian Benteke kuonekana na miili mikubwa zaidi yake lakini ni nyota huyo aliyeipigia hat trick timu yake ya Chelsea kwenye mchezo uliopita wa ligi ya England ndiye anayemaliza sahani yake ya chakula.
Chef huyo anasema mwili mkubwa hauna maana kuwa ndiye anakula sana lakini Hazard ndiye kwenye kikosi cha timu ya Taifa anakula msosi zaidi.
Anasema Romelu Lukaku,ambaye amejengeka na mwili mkubwa ni muangalifu zaidi wa kile anachokula anakula zaidi matunda na Pasta.
Anaongeza kuwa Hazard anapenda kula wala sio siri na aliwahi kuonekana akila burger wakati wa mchezo wa kuisaka tiketi ya fainali za Ulaya 2012 dhidi ya Luxemburg wakati alipopumzishwa na kocha Georges Leekens.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.