Friday, February 28, 2014
Eto'o avunja ukimya baada ya kuitwa babu
Mshambuliaji Samuel Eto'o amecheka taarifa za kocha wake wa Chelsea José Mourinho kuhoji juu ya umri wake akikejeli kama aliweza kupiga hat-trick dhidi ya Manchester United akiwa na miaka 37 basi bado ana miaka mingine mingi ya kutumbukia wavuni.
Jumatano jioni the Blues walitoka sare ya bao 1-1 na Galatasaray kwenye Champions League huku mchezo huo ukiwa umegubikwa na taarifa za Mourinho kuhoji umri wa Eto’o baada ya kuona hatumbukii wavuni ipasavyo pamoja na washambuliaji wenzake.
Baada ya mchezo dhidi ya Galatasaray Eto’o alipohojiwa akasema,yeye ni Samuel Eto'o,atasema nini Zaidi,kama anaweza kufunga mabao matatu dhidi ya Manchester United akiwa na umri wa miaka 36 na 37 ina maana anaweza kuendelea kutumbukia wavuni hata akiwa na miaka 50.
Anasema kwake hajali muhimu kwake ni kujitoa katika timu,kuisaidia na kushinda mataji.
Eto’o anasema anajisikia vizuri,uhusiano wake na kocha ni mzuri na kwake anaendelea kutabasamu,kupigana,kufanya mazoezi vizuri na mambo yatakuwa sawa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.