Manchester United na Chelsea zinapigana vikumbo ili kumnasa mshambuliaji mwenye thamani ya paundi milioni 54 Edinson Cavani wakati wa majira ya joto.
Muwakilishi wa mshambuliaji huyo raia wa Uruguay alikuwa London kuweka mambo sawa wakati huu wakifikiria kuondoka Paris Saint-Germain,ambako Cavani bado hajatulia.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 ana mafanikio huko Ufaransa lakini hana raha kutokana na kuchezeshwa tofauti na mshambuliaji wa kati anakochezeshwa Zlatan Ibrahimovic.
Bosi wa Manchester United David Moyes katika orodha yake limo pia jina la Cavani lakini anajua kuwa atakumbana na upinzani kutoka kwa Jose Mourinho wa Chelsea.
JKlabu zote hizo zinataka kuimarisha safu zao za ushambuliaji huku pia mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa na yule wa Bayern Munich Mario Mandzukic wakitajwa kuwemo kwenye mipango ya kutua kwenye klabu hizo.
Cavani yuko tayari kufanya mazungumzo ya awali wakati huu akiwa nje ya uwanja kwa wiki tatu kwakuwa ni majeruhi na ikielezwa dau lake haliwezi kuwa chini ya paundi milioni 54 zilizolipwa kwa Napoli.
Moyes amewaonya wachezaji wa United watarajie ushindani mkubwa wakati Chelsea wanaweza kumuuza Demba Ba na inawezekana pia Samuel Eto’o na Fernando Torres.
United wanaweza kufikiria ofa kwa Javier Hernandez ambaye anawaniwa na Borussia Dortmund.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.