Wednesday, February 19, 2014

VISINGIZIO : Barcelona walibebwa


BOSS wa Manchester City Manuel Pellegrini amemtupia zigo la lawama muamuzi wa mchezo wao wa jana wa ligi ya mabingwa MSweden Jonas Eriksson akimtuhumu kuwabeba Barcelona wakati timu yake ilipokubali kichapo cha mabao 2-0 ikiwa nyumbani Etihad.

Kocha huyo anamtuhumu Eriksson kwa kutoa penati na kumuonesha kadi nyekundu beki Martin Demichelis.
Anasema muamuzi huyo ndiye aliyeamua matokeo ya mchezo huo akisema aliegemea upande wa Barcelona.

Pellegrini alizungumza na refa huyo baada ya mchezo na kumuangushia tuhuma zake hizo akisema bila shaka atakuwa na furaha kwakuwa yeye ndiye ameamua matokeo hayo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.