Mwanadada raia wa Ethiopia Genzebe Dibaba ameweka rekodi ya dunia ya mashindano ya ndani(Indoor) ya mita 3,000 akiweka rekodi ya zaidi ya sekunde 7 huko Stockholm.
Dibaba, 22,amekimbia kwa dakika 8 na sekunde 16.60 na kuivunja rekodi ya awali ya dakika 8:23.72 iliyowekwa mwaka 2007 na Meseret Defar.
Ndio muda mdogo zaidi katika mbio za mita elfu 3 za ndani(Indoor) na za nje(Outdoor) tangu mwaka 1993,ambapo ni wachina Wang Junxia, Qu Yunxia na Zhang Linli ndio pekee wamewahi kukimbia kwa kutumia muda mchache ambayo sasa rekodi hiyo inashikiliwa na Dibaba.
Dibaba,ndugu wa mshindi mara tatu medali ya dhahabu ya Olympic Tirunesh,pia Jumamosi alivunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 1500.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.