Wednesday, February 26, 2014

Mashabiki wa Simba wamshambulia Ngassa...akoga matusi,mwenyewe akaa kimya

Mshambuliaji wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Tanzania bara na timu ya Taifa ya Tanzania Mrisho Khalfan Ngassa amejikuta akikoga matusi kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kuweka picha tofauti zinazomuonesha akiwa na jezi ya Yanga na nyingine wakati alipokuwa Simba lakini zikiwa na mtazamo tofauti.

Picha aliyova jezi ya Yanga inamuonesha ametandaza misosi huku akiwa na furaha kubwa wakati ile aliyovaa jezi ya Simba anaonekana akipiga miayo kitu kilichofanya mashabiki waanze kuporomosha meneno mazito ikisadikika kuwa ni mashabiki wa Simba wakati wale wanaoonekana kuwa upande wa Yanga wakimpongeza na kummwagia sifa.

Shuka nayo ujionee.
 
 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.