Wednesday, February 19, 2014
Mke na mume washinda medali Olympic
Mke na mume wameshinda medali kwenye Olympic ya majira ya baridi katika michezo ya kuteleza kwenye barafu huko Sochi.
MRussia Alena Zavarzina, 24,amejinyakulia medali ya shaba kwa upande wa wanawake kabla ya dakika 10 baadaye mume wake Vic Wild ,27,kushinda medali ya dhahabu kwa upande wa wanaume.
Wild mzaliwa wa Marekani lakini alibadili uraia na kuchukua ule wa Russia baada ya kumuoa Zavarzina mwaka 2011.
Itakumbukwa mwaka uliopita alishinda medali ya shaba kwenye mashindano ya dunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.