Friday, February 7, 2014

Vidic atangaza rasmi kuondoka United

 Nahodha wa Manchester United Nemanja Vidic ataondoka kwenye timu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

Beki huyo raia wa Serbia mwenye miaka 32 ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu alianza kuitumikia United mwaka 2006 na amezungumza kupitia mtandao wa United na kusema wazi kuwa hafikirii kubaki England na anataka kwenda kupata changamoto nyingine mpya baada ya kushinda mataji yapatayo 15 akiwa na United.

Vidic,ambaye uhamisho wake wa paundi milioni 7 kutua Old Trafford akitokea Spartak Moscow ulitangazwa siku ya sikukuu ya Christmas 2005 aliingoza United kunyakuwa taji lake la kihistoria la ligi kuu,likiwa ni taji la 20 kwa kikosi hicho.

Beki huyo anasema amekuwa na miaka nane safi yenye historia lakini jambo kubwa ambalo hawezi kulisahau ni kuifunga Chelsea kwenye champions league 2008 na kunyakuwa taji hilo huko Moscow.

Vidic akiwa na Man Utd

  • 25 Dec, 2005: Alitua akitokea Spartak Moscow
  • 25 Jan, 2006: Alianza kucheza v Blackburn
  • Premier League titles: 5
  • Champions League: 1
  • League Cup: 3

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.