Friday, February 28, 2014
Eto'o avunja ukimya baada ya kuitwa babu
Mshambuliaji Samuel Eto'o amecheka taarifa za kocha wake wa Chelsea José Mourinho kuhoji juu ya umri wake akikejeli kama aliweza kupiga hat-trick dhidi ya Manchester United akiwa na miaka 37 basi bado ana miaka mingine mingi ya kutumbukia wavuni.
Jumatano jioni the Blues walitoka sare ya bao 1-1 na Galatasaray kwenye Champions League huku mchezo huo ukiwa umegubikwa na taarifa za Mourinho kuhoji umri wa Eto’o baada ya kuona hatumbukii wavuni ipasavyo pamoja na washambuliaji wenzake.
Baada ya mchezo dhidi ya Galatasaray Eto’o alipohojiwa akasema,yeye ni Samuel Eto'o,atasema nini Zaidi,kama anaweza kufunga mabao matatu dhidi ya Manchester United akiwa na umri wa miaka 36 na 37 ina maana anaweza kuendelea kutumbukia wavuni hata akiwa na miaka 50.
Anasema kwake hajali muhimu kwake ni kujitoa katika timu,kuisaidia na kushinda mataji.
Eto’o anasema anajisikia vizuri,uhusiano wake na kocha ni mzuri na kwake anaendelea kutabasamu,kupigana,kufanya mazoezi vizuri na mambo yatakuwa sawa.
Nani zaidi Drogba vs Torres,Eto'o,Ba
Nani zaidi kati ya washambuliaji hawa wenye kiwango cha dunia.
1.Didier Drogba
2.Fernando Torres na Samuel Eto'o
3.Demba Ba
1.Didier Drogba
2.Fernando Torres na Samuel Eto'o
3.Demba Ba
West Brom yamtia kitanzini Anelka,yamtoa kikosini,kisa ishara ya kinazi
West Bromwich Albion imemsimamisha mshambuliaji wake Nicolas Anelka baada ya kufungiwa mechi 5 na kupigwa faini ya paundi elfu 80 kutokana na kushangilia kwa ishara ya kinazi.
Anelka, 34, alikataa kutumia ishara isiyoruhusiwa katika mchezo ambao timu yake ya West Brom ilitoka sare na West Ham December 8.
West Brom wamemsimamisha mpaka hapo baada ya matokeo ya rufaa na mapitio ya klabu kwakuwa Anelka anafikiria kukata rufaa juu ya hukumu hiyo ya FA.
Mfaransa huyo na timu yake ya sharia wametetea ishara hiyo ya ushangiliaji ambapo amesema ilikuwa ni katika kumuunga mkono rafiki yake mchekeshaji wa Ufaransa Dieudonne M'bala M'bala.
Ishara hiyo ya ushangiliaji ambayo aliionesha alipofunga bao la tatu na kufanya mchezo kuwa sare ya mabao 3-3 ilielezewa na Waziri mkuu wa Ufaransa Valerie Fourneyron kuwa ni mbaya na ya kushtua.
Jambo hilo pia liliwafanya wadhamini Zoopla,kutangaza kujitoa kuidhamini timu hiyo.
Thursday, February 27, 2014
Mpenzi wa zamani aibuka,asema eti Eto'o ni kibabu!
Suala la umri mkubwa kwa mshambuliaji wa Chelsea raia wa Cameroon Samuel
Eto'o limechukua sura mpya baada ya mpenzi wa zamani kujitokeza na
kushindilia msumari mwingine.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikaririwa na moja ya vyombo vya habari vya nchini Ufaransa akisema tatizo la timu yake ya Chelsea ni washambuliaji ambao hawatumbukii wavuni kwakuwa wana umri tofauti na ule unaofahamika akitolea mfano akisema Eto'o ana miaka 32 lakini inawezekana ana miaka mitatu zaidi ya hiyo ambayo inatajwa,japo Mourinho mwenyewe amesema suala hilo alilizungumza kiutani na mtu ambaye hajui mpira huku wakicheka lakini akashangaa kupelekwa kwenye vyombo vya habari.
Sasa kama hiyo haitoshi mpenzi wake wa zamani na mama wa mtoto wake wa kwanza Anna Barranca mwenye umri wa miaka 43 akifanya kazi ya muda kwenye store inayouza nywele anasema ana ushahidi kuwa mshambuliaji huyo ana miaka zaidi ya aliyotaja wakati anaingia barani Ulaya na anadhani hana miaka 35 ana miaka zaidi ya 39.
Anasema amezaliwa mwaka 1974 ambayo inamfanya awe ana miaka 39 kwasasa lakini hati yake ya kusafiria inaonesha kuwa ana miaka 32.
Kwa wale wanaojiuliza bifu hilo limetokea wapi kwa bibie huyo,inadaiwa kuwa Eto'o alimtelekeza na binti yake ambaye alimpata miaka 11 iliyopita na sasa akimuoa mwanamke raia wa Ivory Coast ambaye ndiko ana mapenzi moto moto.
Habari hii kwa hisani ya www.mamuafrica.blogspot.com,

Wednesday, February 26, 2014
Mashabiki wa Simba wamshambulia Ngassa...akoga matusi,mwenyewe akaa kimya
Mshambuliaji wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Tanzania bara na timu ya Taifa ya Tanzania Mrisho Khalfan Ngassa amejikuta akikoga matusi kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kuweka picha tofauti zinazomuonesha akiwa na jezi ya Yanga na nyingine wakati alipokuwa Simba lakini zikiwa na mtazamo tofauti.
Picha aliyova jezi ya Yanga inamuonesha ametandaza misosi huku akiwa na furaha kubwa wakati ile aliyovaa jezi ya Simba anaonekana akipiga miayo kitu kilichofanya mashabiki waanze kuporomosha meneno mazito ikisadikika kuwa ni mashabiki wa Simba wakati wale wanaoonekana kuwa upande wa Yanga wakimpongeza na kummwagia sifa.
Shuka nayo ujionee.

Tuesday, February 25, 2014
Mourinho afedheheshwa
Kocha wa timu ya Chelsea ya England, Jose Mourinho ameshutumu tabia ya kurekodi kwa siri mazungumzo yake kuhusu wachezaji wa timu hiyo.
Mourinho amesema lilikuwa jambo la aibu kuona kwamba mazungumzo binafsi kuhusu wachezaji wa timu yake, yanawekwa hadharani na kampuni moja ya televisheni nchini Ufaransa.
Mourinho amesema alikuwa anatania alipokuwa akilalamika kuwa Chelsea inakosa wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji na alimtania Eto'o kuhusu umri wake.
Anasema yalikuwa mazungumzo ya utani na mtu ambaye hahusiki na masuala ya ulimwengu wa soka na kwake anaona fedheha kwa mtu kurekodi mazungumzo binafsi.

Mayweather ulingoni na Maidana
Bingwa wa dunia wa WBC uzito wa welter Floyd Mayweather atashuka ulingoni kupigana na bingwa wa WBA Marcos Maidana pambano litakalofanyika May 3.
Mayweather, 37,mwenye rekodi ya kutopoteza pambano aliuliza mashabiki kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuchagua apigane na bondia gani kati ya Amir Khan na Maidana.
Kutokana na kura za mashabiki sasa atapigana na Maidana mwenye miaka 30 raia wa Argentina.

Thursday, February 20, 2014
Uefa Champions league : Wamepigika
Wednesday, February 19, 2014
VISINGIZIO : Barcelona walibebwa
BOSS wa Manchester City Manuel Pellegrini amemtupia zigo la lawama muamuzi wa mchezo wao wa jana wa ligi ya mabingwa MSweden Jonas Eriksson akimtuhumu kuwabeba Barcelona wakati timu yake ilipokubali kichapo cha mabao 2-0 ikiwa nyumbani Etihad.
Kocha huyo anamtuhumu Eriksson kwa kutoa penati na kumuonesha kadi nyekundu beki Martin Demichelis.
Anasema muamuzi huyo ndiye aliyeamua matokeo ya mchezo huo akisema aliegemea upande wa Barcelona.
Pellegrini alizungumza na refa huyo baada ya mchezo na kumuangushia tuhuma zake hizo akisema bila shaka atakuwa na furaha kwakuwa yeye ndiye ameamua matokeo hayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)