Thursday, April 10, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE : Chelsea yamzuia kipa wake Courtois kuichezea Atletico


Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo amethibitisha kuwa golikipa wao namba moja Thibaut Courtois hatacheza dhidi ya Chelsea,kama klabu hizo zikijikuta zinapangwa kucheza kwenye nusu fainali ya champions league.

Courtois yupo kwenye msimu wake wa tatu akicheza kwa mkopo huko Vicente Calderon akitokea Chelsea.

Hakuna kinachomzuia Courtois kucheza dhidi ya klabu yake ya Chelsea kwakuwa hakuna kipengele kinachomzuia kucheza kama inavyokuwa kwenye ligi kuu lakini Chelsea wameweka kipengele kwenye mkataba wao na Atletico cha kuitaka klabu hiyo kuwalipa fedha Zaidi endapo watamtumia kwenye mchezo ambao timu hizo zinakutana.

Ripoti zinasema dau ambalo Chelsea imeweka kwenye mkataba wake ni wa zaidi ya paundi milioni 4 na nusu.

Rais huyo wa Atletico amesema kiasi hicho ni kikubwa kwao hivyo kama watakutana na Chelsea kivyovyote kipa huyo atakaa nje ya dimba.

Kama Atletico watapangwa kucheza na Chelsea,na Courtois kutocheza hiyo ina maana klabu hiyo ya Hispania itamtumia kipa wake chaguo la pili mwenye umri wa miaka 34 Dani Aranzubia,ambaye amecheza mchezo mmoja msimu huu.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.