Wednesday, April 2, 2014

FIFA yaipiga stop Barcelona kusajili

Mabingwa wa Hispania Barcelona wamefungiwa miezi 14 kufanya uhamisho wa wachezaji na FIFA kwa kuvunja sheria za usajili kusajili wachezaji wa kimataifa chini ya miaka 18.

Klabu hiyo ya Catalan hawawezi kununua wala kuuza mchezaji mpaka 2015 ikiwa na maana hawatasajili wala kuuza kwa vipindi viwili vya usajili.

Pia wamelimwa faini ya paundi 305,000 huku Shirikisho la soka la Hispania nalo likikumbana na adhabu kama hiyo.

Barcelona walikuwa wanataka kusajili kipa mwingine kwaajili ya msimu ujao baada ya kipa wake namba moja Victor Valdes kutangaza kuondoka Nou Camp mwishoni mwa msimu.

Mabingwa hao mara nne wa Ulaya wanahusishwa kutaka kumsajili kipa wa Borussia Monchengladbach Marc-Andre ter Stegen, wakati wamekubali kusajili kiungo mwenye chini ya miaka 17 raia wa Croatia Alen Halilovic wiki iliyopita.

Sheria za FIFA zinaruhusu kusajili mchezaji wa kimataifa mwenye zaidi ya miaka 18 na kama unasajili mchezaji wa aina hiyo wa chini ya miaka 18 unalazimika kufikia vigezo vinavyotakiwa.


Mchezaji mwenye umri chini ya miaka 18 anaruhusiwa kusajiliwa kwenye klabu ya nje ya nchi yake kama wazazi wake watapata uhamisho ambao auhusiani na mambo ya soka,pia kama anaishi km 100 kutoka kwenye klabu iliyomsajili na kama anatokeo kwenye taifa lingine ndani ya umoja wa Ulaya au eneo la kiuchumi Ulaya.

Mapema mwaka huu Barcelona walihusishwa kukwepa kodi katika usajili wa kimagumashi wa Neymar na bado uchunguzi ukiendelea jambo lililosababisha Rais wa klabu hiyo Sandro Rosell kujiuzulu.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.