Tuesday, April 29, 2014

UBAGUZI : Alves kutupiwa ndizi uwanjani Rais wa Brazil aingilia,nyota kibao wamuunga mkono


Rais wa Brazil Dilma Vana Rousseff, amesifu kitendo cha mchezaji wa Brazil, anayekipiga Barcelona Dani Alves kuamua kupotezea kitendo cha ubaguzi wa rangi alichofanyiwa kwa kuamua kuchukua ndizi aliyotupiwa kisha kuimenya na kuila na kuendelea na mchezo ambao timu yake ilikuwa ikicheza dhidi ya Villareal .

Rais Rousseff aliandika katika mtandao wake wa twitter kuwa Dani Alves alionyesha ujasiri wa kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika soka akisema ni tukio la kuigwa .

Klabu ya Villarreal yenyewe imesema imempiga marufuku shabiki aliyefanya kitendo hicho cha kutupa ndizi uwanjani kutohudhuria mechi zote za nyumbani katika maisha yake yote.
Mamia ya watu na wachezaji maarufu duniani wameonyesha upendo wao kwa mchezaji huyo kwa kuweka picha zao kwenye mitandao wa kijamii wakila ndizi.

Rais wa Fifa sepp Blatter naye amepaza sauti yake katika tukio hilo akisema si kitendo kizuri kuendelea kufanyika katika karne hii.

Alves baada ya mchezo alitaka kumshukuru shabiki huyo kwa kumrushia ndizi akisema kama angemfahamu angekwenda kumpa pongezi zake kwakuwa ndizi hiyo ilimpa nguvu ya kupiga krosi mbili ambazo zilizaa mabao yao.

Kitendo ambacho amekifanya beki huyo kimeungwa mkono na wachezaji wengi wakiwemo Sergio Aguero, David Luiz, Oscar, Willian, Nacer Chadli, Moussa Dembele, Hulk na Neymar.
Wachezaji wa Chelsea raia wa Brazil Emboaboa Oscar, David Luiz na Willian wameweka video kwenye account ya Instagram ya Luiz ikiwaonesha wanakula ndizi huku wanasema maneno ya sisi wote ni nyani.

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero yeye ameweka picha kwenye mtandao wa Twitter akiwa na mchezaji soka mwanamke wa Brazil Marta ikiwaonesha wanakula ndizi akiisindikiza na maneno ya Ubaguzi hapana,wote ni sawa.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.