Kocha wa Manchester United David Moyes ametimuliwa kazi baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miezi 10 akirithi mikoba ya Sir Alex Ferguson huko Old Trafford.
Moyes, 50, alichaguliwa na Ferguson baada ya kustaafu kwenye klabu hiyo aliyoitumikia kwa miaka 26.
Taarifa ya klabu imemshukuru Moyes kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa wakati wote akiifundisha klabu hiyo ambayo inakamata nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi kuu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.