Tuesday, April 1, 2014

Murray kutangaza kocha mpya kesho

Mchezaji number moja kwa ubora Uingereza Andy Murray amesema atamtangaza kocha wake mpya kesho.

MScot huyo ambaye aliachana na Ivan Lendl mwezi uliopita akiwa chini ya kocha huyo ameshinda US Open,Wimbledon na taji la Olympic.

Miongoni mwa majina yanayohusishwa kuchukua nafasi hiyo ni mchezaji tennis wa zamani namba moja duniani Mats Wilander, Darren Cahill,ambaye aliwahi kumfundisha Andre Agassi,na Leon Smith,kocha wa timu ya taifa ya Uingereza kwenye Davis Cup.

Lendl,bingwa mara nane wa Grand Slam alichaguliwa kuwa kocha wa Murray mwezi December 2011 kwa lengo la kumuongezea uzoefu na elimu ambayo wengi hawana hasa katika mashindano makubwa.

Katika mwaka wake wa kwanza akiwa na Lendl, Murray alimshinda MSwitzerland Roger Federer kwenye fainali ya Olympic huko London 2012 kabla ya kumshinda MSerbia Novak Djokovic na kushinda 2012 US Open.

Mwaka uliofuata Murray akamaliza ukame wa miaka 77 kwa Uingereza kutopata taji la mmoja mmoja la Wimbledon akipata ushindi mbele ya Djokovic.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.