Monday, April 14, 2014

Pacquiao amtaka Mayweather


Manny Pacquiao ana matumaini ya kucheza pambano na bondia mwenye rekodi ya kutopoteza pambano Floyd Mayweather baada ya kushinda taji la WBO uzito wa welter.

MFilipino, 35, amemshinda Timoth Bradley pambano lililofanyika Las Vegas usiku wa kuamkia jana.

Pacquiao, amegusia uwezekano wa kucheza na Maywether bingwa wa WBC uzito wa welter akisema milango iko wazi kwa pambano hilo.

Anasema kama mpinzani wake atakuwa tayari kupigana naye yuko radhi kucheza pambano hilo.

Pacquiao na Mayweather wanatajwa kama mabondia bora kwa kizazi chao.

Baadaye mwaka huu Pacquiao anatarajiwa kucheza pambano na mshindi kati ya Juan Manuel Marquez na Mike Alvarado ambao watacheza May 17.

Amewahi kucheza na Marquez mara nne na alichapwa mara ya mwisho walipokutana December 2012.

Mayweather, 37, kwa upande wake anashuka ulingoni May 3 kucheza dhidi ya bondia wa Argentina Marcos Maidana.
Head-to-head
Pacquiao

Mayweather
56
Wins
45
5
Losses
0
2
Draws
0

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.