Wednesday, April 23, 2014

MAJANGA : Terry,Cech kukosa mechi zote zilizosalia za msimu


Nahodha wa Chelsea John Terry na golikipa Petr Cech watakosa mechi zote zilizosalia za ligi kuu baada kuumia kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa hapo jana usiku.

Terry alitolewa baada ya kuumia mguu wakati Cech aliumia bega katika mchezo uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Kocha Jose Mourinho amesema Terry anaweza kucheza katika fainali kama timu hiyo itafanikiwa kukata tiketi ya kutinga hatua hiyo mechi itakayopigwa May 24 huko Lisbon.

Lakini watakosa mechi zote za ligi ya EPL ambayo inamalizika May 11.

Cech, 31,alitolewa dakika ya 18 kufuatia kugongana na Raul Garcia wa Atletico na nafasi yake ikachukuliwa na Mark Schwarzer,41,ambaye ilikuwa mechi yake ya kwanza kucheza champions league naye Terry alitolewa zikiwa zimebaki dakika 18 mchezo kumalizika na nafasi yake ikachukuliwa na Andre Schurrle.
Mourinho tayari alikuwa bila ya wachezaji kadhaa kwenye mchezo huo wa jana,mshambuliaji Samuel Eto'o na kiungo Eden Hazard wote ni majeruhi wakati beki Branislav Ivanovic anatumikia adhabu.

Kwa mchezo ujao utakaopigwa Jumatano Chelsea pia itawakosa Frank Lampard na John Mikel Obi ambao watakuwa wanatumikia adhabu ya kadi za njano.
 

Chelsea mechi ilizobaki nazo msimu huu kabla ya fainali ya UCL
  • Sun 27 April: v Liverpool (A)
  • Weds 30 April: v Atletico Madrid (H)
  • Sat 3 May: v Norwich (H)
  • Sun 11 May: v Cardiff (A)

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.