AZAM FC, mabingwa wa Tanzania Bara wameingia Mkataba wa mwaka mmoja na Nahodha wa Burundi, Didier Kavumbangu wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mwingine, iwapo atafanya vizuri katika mwaka wake wa kwanza.
Mshambuliaji huyo aliyemaliza Mkataba wake wa miaka miwili na waliokuwa wapinzani wakuu wa Azam FC katika mbio za ubingwa msimu huu, Yanga SC, amesaini mchana wa leo mbele ya Katibu Mkuu wa klabu, Nassor Idrisa makao makuu ya klabu, Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Katibu Nassor alisema; “Tumepata mshambuliaji mzuri, ambaye tayari ana uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ya Tanzania kwa misimu miwili, mchezaji huyu ni chaguo la kocha wetu Joseph Omog, ambaye alivutiwa naye baada ya kumuona akichezea klabu yake zamani, Yanga SC,”alisema.
Kwa upande wake, Kavumbangu alisema; “Mimi ni mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini viongozi hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini,”.
Mshambuliaji huyo mrefu mwenye nguvu amesema sasa akili yake anaipeleka kwa mwajiri wake mpya, Azam FC ambako pia amepania kwenda kushinda mataji na kuiwezesha timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.
“Mimi sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida yangu huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba moja wa Azam,”amesema.
Kavumbangu alitua Yanga mwaka 2013 akitokea Atletico ya Burundi na katika mechi misimu miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63 za mashindano yote, moja tu la penalti.
Kwa hisani ya mtandao wa AZAM FC
Tuesday, April 29, 2014
WAMERUDI : Chelsea vs Atletico Etoo,Terry Hazard,Cech warudi
Chelsea wamepata nguvu kwenye kikosi chao kuelekea mchezo wa kesho wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Atletico Madrid baada ya Eden Hazard, Petr Cech, John Terry na Samuel Eto'o kufanya mazoezi ya leo.
Hazard,ambaye Jumapili ametajwa kama mchezaji bora chipukizi na chama cha wachezaji wa kulipwa PFA na Eto'o walikosa mchezo wa kwanza uliomalizika kwa syluhu ya bila kufungana wakati Cech na Terry walitolewa kwa kuumia kwenye mchezo huo wa kwanza uliochezwa Vicente Calderon.
Kupitia mtandao wa kijamii wa twitter ya klabu hiyo umesema kuwa wachezaji hao wote wamehudhuria kwenye mazoezi kwenye viwanja vya Cobham.
UBAGUZI : Alves kutupiwa ndizi uwanjani Rais wa Brazil aingilia,nyota kibao wamuunga mkono
Rais wa Brazil Dilma Vana Rousseff, amesifu kitendo cha mchezaji wa Brazil, anayekipiga Barcelona Dani Alves kuamua kupotezea kitendo cha ubaguzi wa rangi alichofanyiwa kwa kuamua kuchukua ndizi aliyotupiwa kisha kuimenya na kuila na kuendelea na mchezo ambao timu yake ilikuwa ikicheza dhidi ya Villareal .
Rais Rousseff aliandika katika mtandao wake wa twitter kuwa Dani Alves alionyesha ujasiri wa kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika soka akisema ni tukio la kuigwa .
Klabu ya Villarreal yenyewe imesema imempiga marufuku shabiki aliyefanya kitendo hicho cha kutupa ndizi uwanjani kutohudhuria mechi zote za nyumbani katika maisha yake yote.
Mamia ya watu na wachezaji maarufu duniani wameonyesha upendo wao kwa mchezaji huyo kwa kuweka picha zao kwenye mitandao wa kijamii wakila ndizi.
Rais wa Fifa sepp Blatter naye amepaza sauti yake katika tukio hilo akisema si kitendo kizuri kuendelea kufanyika katika karne hii.
Alves baada ya mchezo alitaka kumshukuru shabiki huyo kwa kumrushia ndizi akisema kama angemfahamu angekwenda kumpa pongezi zake kwakuwa ndizi hiyo ilimpa nguvu ya kupiga krosi mbili ambazo zilizaa mabao yao.
Kitendo ambacho amekifanya beki huyo kimeungwa mkono na wachezaji wengi wakiwemo Sergio Aguero, David Luiz, Oscar, Willian, Nacer Chadli, Moussa Dembele, Hulk na Neymar.
Wachezaji wa Chelsea raia wa Brazil Emboaboa Oscar, David Luiz na Willian wameweka video kwenye account ya Instagram ya Luiz ikiwaonesha wanakula ndizi huku wanasema maneno ya sisi wote ni nyani.
Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero yeye ameweka picha kwenye mtandao wa Twitter akiwa na mchezaji soka mwanamke wa Brazil Marta ikiwaonesha wanakula ndizi akiisindikiza na maneno ya Ubaguzi hapana,wote ni sawa.
Wednesday, April 23, 2014
MAJANGA : Terry,Cech kukosa mechi zote zilizosalia za msimu
Nahodha wa Chelsea John Terry na golikipa Petr Cech watakosa mechi zote zilizosalia za ligi kuu baada kuumia kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa hapo jana usiku.
Terry alitolewa baada ya kuumia mguu wakati Cech aliumia bega katika mchezo uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Lakini watakosa mechi zote za ligi ya EPL ambayo inamalizika May 11.
Cech, 31,alitolewa dakika ya 18 kufuatia kugongana na Raul Garcia wa Atletico na nafasi yake ikachukuliwa na Mark Schwarzer,41,ambaye ilikuwa mechi yake ya kwanza kucheza champions league naye Terry alitolewa zikiwa zimebaki dakika 18 mchezo kumalizika na nafasi yake ikachukuliwa na Andre Schurrle.
Mourinho tayari alikuwa bila ya wachezaji kadhaa kwenye mchezo huo wa jana,mshambuliaji Samuel Eto'o na kiungo Eden Hazard wote ni majeruhi wakati beki Branislav Ivanovic anatumikia adhabu.
Kwa mchezo ujao utakaopigwa Jumatano Chelsea pia itawakosa Frank Lampard na John Mikel Obi ambao watakuwa wanatumikia adhabu ya kadi za njano.
Chelsea mechi ilizobaki nazo msimu huu kabla ya fainali
ya UCL
- Sun 27 April: v Liverpool (A)
- Weds 30 April: v Atletico Madrid (H)
- Sat 3 May: v Norwich (H)
- Sun 11 May: v Cardiff (A)
Subscribe to:
Posts (Atom)