Friday, November 7, 2014

TBL wataka kuvunja mkataba wa Taifa Starz kisa ni ripoti ya ubadhirifu TFF



Rais wa Shirikisho la kabumbu hapa nchini TFF Jamal Emil Malinzi amebainika kuwapigia goti wadhamini wa Taifa Starz bia ya Kilimanjaro ambao waliweka bayana nia yao ya kuvunja mkataba kufuatia ufujaji wa pesa za udhamini.

Malinzi amewataka wadhamini hao kuwa na subira huku akitumia kivuli cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Starz na timu ya Taifa ya Vijana zilizokuwa zinakabiliwa na mechi za kuisaka tiketi ya kucheza fainali za Africa.

Kutaka kuvunjwa kwa mkataba huo kumetokana na ripoti ya ukaguzi kuonesha kuwa kuna ufujaji wa pesa za udhamini unaofanywa na TFF huku matumizi mengine yakiwa hayana maelezo yoyote.

Kwa mujibu wa mkataba kipengele cha 4.1 kinasema wazi kuwa TFF haitakiwi kufanya matumizi yoyote ya pesa za udhamini bila ya kukaa na kukubaliana na wadhamini wao lakini TFF imekwenda kinyume cha hapo ikifanya matumizi bila ya kuwashirikisha wadhamini tena matumizi ambayo hayana maelezo yanaonesha kuwa ni matumizi halali.

Ripoti ya ukaguzi imesema wazi kuwa kuna kiasi cha dola 381,248 ambazo zimelipwa pasipo makubaliano ikiwa ni moja ya matumizi mabovu ya pesa za udhamini.

Aidha inaonesha kuwa TFF walichota dola elfu 90 ili kulipa fidia kwa kocha waliyemvunjia mkataba Kim Paulsen,wakachota tena dola elfu 34,177 ikiwa ni manunuzi ya Hiace mbili pamoja na pesa nyingine iliyochotwa kwaajili ya malipo kwa mikoa kuendesha zoezi la maboresho ya taifa Starz.

Kama hiyo haitoshi ripoti hiyo inaonesha kuwa ilichotwa dola elfu 10 ambazo alilipwa Malinzi sambamba na kiasi kingine cha dola elfu 15,934 na dola 69,471 na kiasi kingine cha dola 63,735

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.