Tuesday, November 25, 2014
Baada ya ubingwa wa dunia Hamilton ampiga kijembe Rosberg,asema msimu umekwisha kwa heshima
Bingwa wa dunia wa Formula 1 Lewis Hamilton amesema mahusiano yake na dereva mwenzake Nico Rosberg msimu huu yamekuwa magumu kuliko ilivyokuwa na dereva mwenzake Fernando Alonso lakini msimu umekwisha kwa kuheshimiana.
Hamilton, 29, amembwaga Rosberg na kuchukua ubingwa wa dunia baada ya mwezi mzima wa kimuhemuhe na mikwaruzano kati madereva hao wa Mercedes ikiwemo matukio kadhaa kati yao.
Anakumbuka mwaka 2007,alipokuwa akisigana na dereva mwenzake Alonso wakati akiwa na timu ya Mclaren lakini hata hivyo anasema msimu umekwisha huku kukiwa na heshima baina yao.
Hamilton anasema ilikuwa ngumu lakini Rosberg amekuwa tatizo Zaidi japo kwake anasema unahitaji mshindani wa aina hii ili kukupa ushindani mzuri na kukusukuma katika mafanikio.
Akichukua taji hilo kwa mara ya tatu 2015 Hamilton atakuwa sawa na Ayrton Senna,ambaye amechukua taji hilo mwaka 1988, 1990 na 1991.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.