Tuesday, November 25, 2014

James Rodriguez,Nyota Real Madrid aliyeingia anga za Ronaldo



Nyota wa Colombia aliyetua Real Madrid ya Hispania msimu huu James Rodriguez amefuata nyayo za Cristiano Ronaldo na David Beckham baada ya kutangaza hadharani nguo zake za ndani.

Nyota huyo wa Real Madrid ameungana na nembo ya kibiashara ya Colombia ya Bronzini na kuonesha aina zake za nguo hizo za ndani ambazo zinaitwa J10.

Rodriguez amekuwa mmoja wa wachezaji wenye soko kubwa duniani kwa mwaka huu 2014.

Aling’ara Zaidi kwenye fainali za kombe la dunia 2014 zilizofanyika Brazil na kufanikiwa kupata deal ya kusajiliwa na Real Madrid akitokea Monaco ya Ufaransa kwa dau la paundi milioni 63 na kumfanya kuwa mmoja wa wachezaji ghali duniani.

Rodriguez anakuwa mchezaji watatu wa Real Madrid kuingia katika ulimwengu wa fashion,akiwafuatia nahodha wa zamani wa England Beckham na nyota wa Ureno Ronaldo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.