Monday, November 17, 2014
AFCON 2015 yazidi kunoga,wababe nane tayari uhakika
Baada ya mechi zilizopigwa jana za kuisaka tiketi ya kufuzu fainali za Africa mwakani timu nane tayari zimekata tiketi za kucheza katika fainali hizo ambazo zitachezwa huko Equatorial Guinea.
Timu ambazo zimejihakikishia nafasi hiyo ni South Africa, Burkina Faso, Gabon, Cameroon, Cape Verde, Tunisia,Algeria na Senegal.
Katika kundi A South Africa wamefuzu baada ya ushindi wao wa mabao 2-1 wakiishinda Sudan kwa mabao ya Thulani Serero na Tokelo Rantie.
South Africa wamefikisha pointi 11 wakifuatiwa na Nigeria na Congo wenye pointi saba kila mmoja wakati Sudan wana pointi tatu.
Kwenye kundi B Algeria wamepata ushindi wake wa tano katika mechi tano wakiishinda Ethiopia kwa mabao 3-1 dhidi ya Ethiopia na kujihakikishia kucheza katika fainali hizo baada ya kujikusanyia pointi 15.
Kundi C Burkina Faso na Gabon wamejihakikishia nafasi ya kucheza fainali hizo mwakani zikiwa juu ya kundi hilo,Burkina Faso wamefikisha pointi 10 wakati Gabon wamefikisha pointi 9.
Kundi D Cameroon wamefuzu baada ya kufikisha pointi 13 wakifuatiwa na Ivory Coast wenye pointi tisa.
Kunako kundi E bado mambo magumu,Ghana wanaongoza wakiwa na point 8 wakifuatiwa na Uganda wenye pointi 7 ,Togo wana pointi 6 wakiwa nafasi ya tatu na Guinea wana pointi 4.
Kundi F Cape Verde wamefuzu wakiwa na pointi 12 wakifuatiwa na Zambia wenye pointi 8 na Msumbiji wana 5 nao Niger wakiburuza mkia wakiwa na pointi 2.
Kundi G Tunisia na Senegal tayari wamefuzu kwa Tunisia kufikisha pointi 11 huku Senegal wakiwa na pointi 10 nao Misri wako nafasi ya tatu wakiwa na pointi 6 na Botswana wana pointi yao 1 tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.