Thursday, November 13, 2014

Chelsea wamnyatia Bale

Kwa mujibu wa Tuttomercatoweb,Chelsea the Blues wanaangalia uwezekano wa kumnasa Gareth Bale baada ya kuwepo taarifa kuwa haendani na mfumo mpya alioanza kuutumia kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti.
 
Bale alijiunga na klabu hiyo kwa dau lililoweka rekodi ya dunia ya paundi milioni 85 zaidi ya mwaka mmoja uliopita na amekwishafunga mabao 28 katika michezo 58.
 
Pia kiwango cha Isco kimeonekana kuwa tishio kwa nafasi ya Bale katika kikosi cha kwanza ikizingatiwa kuwa Cristiano Ronaldo, Toni Kroos, James Rodriguez na Luka Modric wote wamo kikosi cha kwanza huko Santiago Bernabeu.

Bale anahusishwa kutakiwa huko Old Trafford lakini kama Real watakuwa tayari kumuachia boss wa Chelsea Jose Mourinho atakuwa mmoja wa klabu za kwanza kutangaza ofa yao.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.