Kocha wa KCCA George 'Best' Nsimbe ataendelea kubaki kwa mabingwa hao wa Uganda mpaka january mwakani.
Nsimbe amekubali kujiunga na mabingwa wa Tanzania Azam FC kama kocha msaidizi ambapo kiungo huyo wa zamani wa KCC na timu ya taifa The Cranes aliyefanya mazungumzo na Azam wikiendi iliyopita atakuwa chini ya MCameroon Joseph Marius Omog.
Kocha Nsimbe mwenyewe amethibitisha kumalizana na Azam japo akisema bado anaendelea kuutumikia mkataba wake na KCCA.
Akiwa Tanzania, Nsimbe alishuhudia mchezo wa ligi kuu Azam wakiichapa Coastal Union.
Nsimbe, amefanikiwa kushinda taji la ligi kuu ya Uganda mara mbili mfululizo 2013 na 2014 na anatajwa huenda akatajwa kocha mkuu wa Azam FC kama watamuondoa Omog.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.