Winger wa Mbeya City Deus Kaseke usiku wa kuamkia leo amewahenyesha vigogo vya soka Simba na Yanga wanaotaka saini yake kwa gharama yoyote.
Kaseke yupo jijini Dar Es Salaam kusikiliza ofa ya klabu hizo kongwe ambazo kila mmoja kwa wakati wake anaitaka huduma yake.
Usiku wa kuamkia leo Yanga walipanga na Kaseke wakutane kwenye hoteli moja maeneo ya Masaki ili wafanye mazungumzo na kusikiliza dau lake na ikiwezekana wamalizane kabisalakini hata hivyo aliishia kuwakalisha Yanga bila kutokea.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini na cha uhakika kimesema kuwa Kaseke amefanya mazungumzo kwenye simu na Yanga lakini hakutokea kwenye hoteli waliyoahidiana.
"Unajua sisi tumekubaliana naye tufanye mazungumzo na ikiwezekana tumalizane lakini kila tukimpigia anasema anakuja na hakutokea"kilisema chanzo hicho kutoka ndani ya Yanga.
Wakati Yanga wakimvizia kwa upande wa Simba wanadaiwa kumuweka mafichoni na usiku huo wa kuamkia leo walikuwa na mazungumzo naye mazito ya kuhakikisha anasaini.
Mmoja wa viongozi wa Simba mwenye ushawishi katika usajili na ambaye huwa anasajili wachezaji wakati mwingine kwa pesa yake ndiye aliyekuwa na Kaseke usiku huo pamoja na baadhi ya viongozi wa Simba wakifanya mazungumzo ya kumalizana naye na taarifa za kutoka katika kikao hicho ambazo hata hivyo mabosi wa Simba hawajazithibitisha zinasema kuwa tayari mchezaji huyo amekubali kuachana na Mbeya City na anasaini kuwachezea wekundu hao.
Tunaendelea kufuatilia kwa undani zaidi na kukuletea kile ambacho kinaendelea kujiri katika usajili.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.