Wednesday, November 19, 2014
Sturridge majanga matupu Liverpool
Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya England Daniel Sturridge ameumia tena mazoezini.
Sturridge mwenye miaka 25 ameumia misuli ya paja hapo jana na alitarajiwa kufanyiwa vipimo Zaidi leo Jumatano.
Mshambuliaji huyo ambaye amefunga mabao 25 msimu uliopita amecheza mechi tatu tu za msimu huu katika ligi kuu ya England na alirejea kwenye mazoezi wiki iliyopita.
Aliumia misuli ya paja akiwa na kikosi cha timu ya Taifa mwezi September kabla ya kuumia kigimbi kwenye mazoezi mwezi October na sasa msuli wa paja unamuweka nje.
Liverpool wameshinda mechi nne pekee kati ya 14 wakicheza bila ya mshambuliaji huyo aliyewahi kucheza Chelsea na Manchester City na sasa wakikamata nafasi ya 11.
Kikosi hicho kinachonolewa na Brendan Rodgers wamefunga mabao 14 katika ligi kuu msimu huu huku washambuliaji Mario Balotelli, Fabio Borini na Rickie Lambert wakishindwa kuchungulia nyavu.
Rodgers anaongeza majanga kwenye kikosi chake baada ya mshambuliaji Mario Balotelli naye kuumia misuli ya nyuma ya paja akiwa katika majukumu ya timu ya taifa ya Italia na inawezekana akakosa mchezo unaofuata dhidi ya Crystal Palace utakaopigwa Jumapili November23.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.