Thursday, November 13, 2014

Drogba "Out" Chelsea

DIDIER DROGBA anaweza kuondoka Chelsea ifikapo mwisho wa msimu wakati kocha Jose Mourinho akisaka saini ya kinda Anderson Talisca.


Drogba mwenye miaka 36 aliyerejea tena Chelsea na kusaini mkataba wa miezi 12 anatajwa kuweza kuondoka kwenye klabu hiyo kama Mourinho ataipata saini ya Talisca.


Kinda huyo amekuwa pia anatupiwa jicho na klabu za Arsenal na Liverpool.
 
Akiwa na miaka 20 anaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza kama kiungo mshambuliaji na kama mshambuliaji na kama mourinho ataipata saini yake,itamsukuma Drogba nje ya kikosi hicho.
 
Drogba mwenyewe anasema bado mkataba wake haujaisha Chelsea na kikubwa anataka kushinda mataji na kuweka historia tena huko darajani.
 
Anasema mahusiano yake na mashabiki ni mazuri kwa pande zote na anasema miaka nane aliyoitumikia klabu hiyo hapo kabla ilikuwa bora katika maisha yake ya soka na anafahamu kuwa mashabiki nao walifurahishwa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.