Monday, October 27, 2014

Nahodha timu ya Taifa auwa kwa kupigwa risasi,kisa ni kumtetea mpenzi


NAHODHA wa Bafana Bafana na Orlando Pirates Senzo Meyiwa ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa akijaribu kumtetea mpenzi wake kuporwa nyumbani kwake karibu na Johannesburg.

Golikipa huyo wa Orlando Pirates mwenye miaka 27 amefariki jana baada ya kupigwa risasi kifuani nyumbani kwa mpenzi wake Kelly Khumalo,ambaye ni muigizaji na muimbaji katika mji wa Vosloorus.

Watu wawili waliingia na kutaka kupewa simu za mkononi,pesa na vitu vingine vya thamani.

Afisa wa usalama katika mji huo Sizakele Nkosi-Malubane amesethibitisha tukio hilo na kusema kuwa Senzo alikuwa akimkinga mpenzi wake ambaye alikuwa amenyooshewa bunduki na mmoja wa watu hao.

Meyiwa alithibitika kufariki alipofikishwa hospitali.

Police nchini humo wamesema watu wawili waliingia katika nyumba hiyo saa 2 usiku wakati mwingine mmoja alikuwa akisubiri nje na wote watatu walikimbia baada ya tukio hilo.

Polisi wamesema kuwa watahakikisha wauaji hao wanakamatwa na tayari zawadi ya randi 150,000 imetangazwa kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji.

Meyiwa aliiongoza Africa Kusini Bafana bafana katika mechi zake nne zilizopita za kuisaka tiketi ya kucheza fainali za Africa mwakani bila kuruhusu goli na Jumamosi aliiongoza timu yake kusonga nusu fainali ya South African League Cup.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.