Wednesday, October 22, 2014

Chelsea majanga..


Jose Mourinho amekumbwa na uhaba wa washambuliaji kunako kikosi chake kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Manchester United utakaopigwa Jumapili.

Licha ya kukabiliwa na uhaba huo wa washambuliaji Mourinho amesema hana wasiwasi wowote na mchezo huo.

Chelsea tayari wapo bila ya Diego Costa aliyeukosa pia mchezo wa ligi ya mabingwa jana usiku dhidi ya Maribor mchezo ambao uliwafanya Chelsea kumpoteza Loic Remy aliyeumia katika dakika ya 16 baada ya kufunga bao la kuongoza.
 
Hiyo inamaanisha sasa Chelsea wanabakiwa na mshambuliaji Didier Drogba pekee ambaye naye hapo jana usiku alifunga bao lake la kwanza tokea amerejea katika timu hiyo.
 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.