Wednesday, October 1, 2014
Di Maria afikiria kuchomoka Man United
Winger mpya wa Manchester United Angel Di Maria anafikiria kutimiza ndoto yake kwa kurejea kucheza soka kwenye taifa lake la asili Argentina.
Di Maria mwenye miaka 26 ambaye ametua Old Trafford kwa dau lililoweka rekodi Uingereza la paundi milioni 59.7 tayari jicho lake limeanza kungazia hatima yake ya baadaye.
Rosario Central,klabu ya kwanza Di Maria kuichezea ndio anayotamani kurejea tena japo hajasema kama anapanga kuondoka lini Manchester United.
Anasema ilikuwa ndoto yake kucheza soka Ulaya na sasa ndoto yake ni kurejea Argentina na kuichezea klabu yake hiyo iliyomkuza.
Anaongeza kuwa timu hiyo siku zote imekuwa ya kwanza kichwani kwake na amezungumza na Ezequiel Lavezzi na Javier Mascherano ili kama kuna uwezekano wote warudi kwenye klabu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.