Tuesday, October 7, 2014

Rais Italia apigwa kifungo miezi sita


Rais wa Shirikisho la soka Italia FIGC, Carlo Tavecchio,amefungiwa miezi sita na UEFA kwa kuzungumza maneno ya kibaguzi.

Rais huyo mwenye miaka 71 alisababisha mkanganyiko wakati wa kampeni za uchaguzi mwezi July kwa kuzungumza maneno ya kibaguzi kwa wachezaji wa kiAfrica kwa kula ndizi.

Kifungo hicho kinamaanisha Tavecchio hawezi kushikilia nafasi yoyote ya UEFA na atajadiliwa katika mkutano mkuu utakaofanyika mwezi March mwakani.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.