Tuesday, November 25, 2014

Berahino akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa


Mshambuliaji wa West Bromwich Albion na England mwenye asili ya Burundi Saido Berahino atawekwa kikaangoni na kuhojiwa baada ya kukamatwa akiendesha gari akiwa amelewa.

Mchezaji huyo ambaye anang’ara kwasasa alikamatwa October 22 ikiwa ni siku mbili tokea amefunga katika mchezo ambao timu yake ilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Manchester United huku yeye akitupia wavuni.

Msemaji wa Polisi amesema mshambuliaji huyo mwenye miaka 21 alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi katika njia isiyoruhusu mwendo huo.

Berahino sasa atarudi tena Polisi kuhojiwa mapema mwezi ujao wa December.

Baada ya ubingwa wa dunia Hamilton ampiga kijembe Rosberg,asema msimu umekwisha kwa heshima


Bingwa wa dunia wa Formula 1 Lewis Hamilton amesema mahusiano yake na dereva mwenzake Nico Rosberg msimu huu yamekuwa magumu kuliko ilivyokuwa na dereva mwenzake Fernando Alonso lakini msimu umekwisha kwa kuheshimiana.

Hamilton, 29, amembwaga Rosberg na kuchukua ubingwa wa dunia baada ya mwezi mzima wa kimuhemuhe na mikwaruzano kati madereva hao wa Mercedes ikiwemo matukio kadhaa kati yao.

Anakumbuka mwaka 2007,alipokuwa akisigana na dereva mwenzake Alonso wakati akiwa na timu ya Mclaren lakini hata hivyo anasema msimu umekwisha huku kukiwa na heshima baina yao.

Hamilton anasema ilikuwa ngumu lakini Rosberg amekuwa tatizo Zaidi japo kwake anasema unahitaji mshindani wa aina hii ili kukupa ushindani mzuri na kukusukuma katika mafanikio.

Akichukua taji hilo kwa mara ya tatu 2015 Hamilton atakuwa sawa na Ayrton Senna,ambaye amechukua taji hilo mwaka 1988, 1990 na 1991.

Mpenzi wa Sanchez atishia kiwango cha nyota huyo,kisa uhitaji wa ngono kwa sana


NYOTA wa Arsenal Alexis Sanchez anaweza kuwa mchovu mapema akiwa na Arsenal ikiwa ni matokeo ya soka la kupitiliza na kufanya mapenzi kwa sana kwa mujibu wa taarifa kutoka nyumbani kwao Chile.

Inaelezwa uchovu huo unatokana na ratiba inayofululiza ya mechi za Arsenal na Timu ya taifa ambayo pia inafanywa kuwa mbaya Zaidi na uhitaji mkubwa wa mapenzi kutoka kwa mpenzi wake Laia Grassi anaporudi nyumbani.
Hata hivyo mpaka sasa kutokuwa na mipaka ya ufanyaji mapenzi na kwenye soka haijaonesha kuathiri kiwango cha Sanchez mwenye miaka 25 akiwa ni mmoja wa wachezaji hatari hata kwenye mchezo uliopita ambao Arsenal walifungwa mabao 2-0 na Manchester United weekend iliyopita alionekana kuwa mwiba zaidi.