Wednesday, November 27, 2013

Ancelotti akiri kutaka "kuua"mchezaji


Boss wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti amekiri kuwa alitamani kumuua mmoja wa wachezaji huko Stamford Bridge.

MTALIANO huyo aliyeiongoza Chelsea kupata mataji mawili Ligi kuu na kombe la FA katika msimu wake wa kwanza huko Magharibi mwa London lakini akatimuliwa mwaka mmoja baadaye.
Lakini wakati Ancelotti anafurahia mahusiano mazuri na wachezaji wakati akiwa the Blues, AC Milan, Paris Saint-Germain na sasa Real Madrid,anakiri kuwa kuna mchezaji mmoja ambaye hakutaka kumtaja ambaye anasema ni tatizo kubwa Stamford Bridge.

Anasema hakuwahi kuwa na matatizo na wachezaji lakini yupo mmoja hakuonesha heshima na alijaribu kummaliza lakini haikuwezekana.
Ancelotti hakutaka kumtaja mchezaji huyo japo anasema aliwahi pia Didier Drogba kwa kuchelewa baada ya kufika dakika 30 kabla ya mechi kuanza na akamuweka benchi lakini anasema mahusiano yao yaliimarika.

Kipigo chaipa Chelsea tiketi ya kusonga mbele,yaendelea kuongoza kundi E

Licha ya kukutana na kipigo cha bao 1-0 kuitoka kwa FC Basel ya Uswis,wazee wa darajani Chelsea wamefuzu hatua ya mtoano ya Champions League.

Hata hivyo kipigo hicho kinawafanya Chelsea kuwa wateja wa FC Basel ambao katika mchezo wa kwanza walipata ushindi wa mabao 2-1 Stamford Bridge huku Mohamed Salah akiwa ni mchezaji aliyefanikiwa kufunga kwenye mechi zote hizo mbili.

Hatua ya Chelsea kufuzu inatokana na Schalke kutoka sare na Steaua Bucharest ya Romania na hivyo kuendelea kuongoza kundi E.


Group E

Pld GD Pts
Chelsea
             5
              8
              9
Schalke
             5
              1
              8
Basel
             5
             -2
              7
Steaua Bucharest
             5
             -7
              3

Tuesday, November 26, 2013

Uefa Champions League mzigoni

Ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya makundi inaendelea leo kuisaka tiketi ya kuelekea kwenye hatua ya mtoano.

Arsenal waliokaa kwenye kundi la mtego watakuwa na kibarua cha kutaka kufanya vizuri ili kujiweka mguu sawa na hatua ya mtoano huku Chelsea nayo ikihitaji matokeo mazuri dhidi ya mbaya wao aliyewafunga kwenye mchezo wa kwanza.

FC Barcelona nao wako mzigoni kama ilivyo kwa Dortmund na Napoli na AC Milan pia dhidi ya Celtic


Mechi za leo

Monday, November 25, 2013

CHALLENGE CUP : Kilimanjaro Stars yaenda Nairobi na matumaini kibao


Timu ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars imeondoka kuelekea nchini Kenya kwa mashindano ya kombe la challenge linalotaraji kuanza kuunguruma November 27.


Kilimanjaro Starz imeondoka na matumaini kibhao ya kurejea na kikombe hicho kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

Wachezaji waliomo katika msafara huo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).

Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Hata hivyo, washambuliaji Samata na Ulimwengu watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba Mosi mwaka huu wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Benchi la Ufundi la timu hiyo linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu), Frank Mhonda (mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).

Kilimanjaro Stars ambayo ipo kundi B katika michuano hiyo itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.

Pacquiao sasa kiu yake ni Floyd Mayweather

Manny Pacquiao sasa yupo tayari kupigana na Floyd Mayweather lakini anasema ni juu ya bondia huyo wa Marekani kuamua lini anataka pambano hilo.

Pacquiao, kutokea Philippines,hapo jana amepata ushindi wake wa kwanza baada ya miaka miwili  baada ya kumshinda Brandon Rios na kunyakuwa taji la WBO uzito wa welter.

Anasema kazi yake ni kupigana kwahiyo yupo tayari kupigana na Mayweather.


Mapambano 10 yaliyopita ya Manny Pacquiao

  • 23 Nov, 2013: v Brandon Rios (US), won (pts)
  • 8 Dec, 2012: v Juan Manuel Marquez (Mex), lost (KO 6th)
  • 9 Jun, 2012: v Timothy Bradley (US), lost (pts)
  • 12 Nov, 2011: v Juan Manuel Marquez (Mex), won (pts)
  • 7 May, 2011: v Shane Mosley (US), won (pts)
  • 13 Nov, 2010: v Antonio Margarito (Mex), won (pts)
  • 13 Mar, 2010: Joshua Clottey (Gha), won (pts)
  • 14 Nov, 2009: v Miguel Cotto (Pue), won (stoppage, 12th)
  • 2 May, 2009: v Ricky Hatton (GB), won (KO, 2nd)
  • 6 Dec, 2008: v Oscar de la Hoya (US), won (retired, 8th)

AVB : Spurs kupigwa sita aibu yetu wenyewe


Kocha wa Tottenham Andre Villas-Boas amesema kikosi chake kinatakiwa kuona aibu kwa kipigo cha mabao 6-0 kutoka kwa Manchester City.

Spurs imekubali kipigo kikubwa kwa mara ya kwanza tokea ilipofungwa 7-1 na Newcastle December 1996.

Kipigo hicho cha jana kimewaacha Spurs kukalia katika nafasi ya tisa wakiwa na point inane nyuma ya wanaoongoza ligi Arsenal.

Villas-Boas amesema kipigo walichokipata ni kikubwa na ambacho wanatakiwa kuona aibu wao wenyewe kwa kukosa umakini na kuruhusu kipigo kikubwa ambacho hawakustahili.

Friday, November 22, 2013

Mourinho ambwatukia mkuu wa waamuzi

Boss wa Chelsea Jose Mourinho amemponda mkuu wa waamuzi Mike Riley kwa kuomba msamaha kwa West Brom kufuatia penati iliyotolewa dakika za mwisho kwenye mchezo wao dhidi ya Chelsea.

Mourinho anamini kitendo cha Riley kinaibua hatari kubwa huku akisema hakuna mtu aliyempigia simu kumuomba radhi kwa bao la pili la West Bromn ambalo mchezaji wa Chelsea Ramires alifanyiwa madhambi na Steven Reid lakini mwamuzi akaacha wakaenda kufunga.

Kocha huyo ameyasema hayo baada ya Riley kupiga simu kwa West Brom kuwaomba radhi kwa penati iliyotolewa na Andre Marriner dakika za lala salama iliyofanya matokeo kumalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.