Super-agent Jorge
Mendes amemwagia sifa mteja wake kocha Jose Mourinho akisema ni yeye pekee
mwenye uwezo wa kuchukua utawala wa Sir Alex Ferguson ambaye ameacha historia
kubwa kwa timu ya Manchester United.
Ferguson,ambaye alishinda mataji 38 katika miaka 26 aliyokuwepo
huko Old Trafford alistaafu mwaka 2013 na nafasi yake ikachukuliwa na David
Moyes ambaye hata hivyo alidumu kwa miezi 10 pekee.
Mendes anasema ni ngumu kumpata mtu kama Ferguson kwasababu
alikuwa ana akili ya ziada na kumtafuta mtu wa aina hiyo ni ngumu lakini
akasema kwa England sasa wana mmoja tu ambaye ni Mourinho.
Anasema Mourinho kwasasa anaweza kufanya hilo kwa Chelsea
kwasababu anawapenda mashabiki,anaupenda mji na anafikiri kuwa taka Zaidi ya miaka
10.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.