Friday, February 6, 2015

Mtoto wa miaka sita ampa ajira Mourinho Villa ParkKIJANA mdogo wa miaka sita mshabiki wa Aston Villa,Jude Branson amemuandikia barua kocha wa Chelsea Jose Mourinho akimuomba kuhamia huko Villa park ili kuinusuru timu hiyo na janga la kushuka daraja huku akimtaka kutua pamoja na mshambuliaji Diego Costa.

Branson,amemtaka kocha huyo kuwakomboa katika kipindi hiki kigumu wanachukutana nacho wakiwa chini ya kocha Paul Lambert.

Katika barua yake dogo huyo amueleza jinsi anavyomzimikia Mourinho akisema ndiye kocha wake kipenzi hivyo akimuomba kuichukua Aston Villa huku akimuomba kutua na Costa.

Aston Villa kesho watakutana uso kwa uso na Chelsea huko Villa Park huku ikiwa imecheza mechi nane bila ushindi na ikicheza kwa saa 10 na dakika 12 bila ya kufunga goli lolote.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.