Wednesday, February 4, 2015

Barcelona washtukia mchezo mchafu wa Real Madrid



RAIS wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amefichua kuwa mahasimu wao Real Madrid wamehusika na mchezo wa uhamisho wa Neymar kiasi cha kutakiwa kuwasilisha ushahidi.

Bartomeu anasema hakuna ujanja walioufanya kwenye usajili huo na siku zote watasimama katika ukweli kwakuwa uhamisho huo ulifanywa chini ya mwanasheria anayeheshimika.

Anasema kuna klabu nyingine zilimtaka Neymar na wakataka kulipa pesa nyingi Zaidi lakini wakashindwa na hilo hawakulipenda.

Ameongeza kuwa baba wa Neymar alimwambia kuwa Neymar kwa wakati huo alikuwa akiwaniwa na klabu mbili tu Barcelona na Real Madrid na wapinzani wao walikuwa tayari kutoa kitita kinene Zaidi.

Bartomeu pia amesema nyuma ya suala ya Neymar kuna kampeni za kisiasa dhidi ya klabu hiyo kuhusiana na kutaka kujitenga na kujitegemea kwa Catalunya.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.