Tuesday, September 9, 2014

FORMULA1 : Rosberg amuangukia Hamilton kimtindo


DEREVA wa Mercedes Nico Rosberg ana matumaini kuwa mashabiki wa Formula 1 wamemsamehe baada ya kuzomewa katika mashindano mawili yaliyopita.

Rosberg alipokewa vibaya na mashabiki baada ya kugongana na Lewis Hamilton ambaye ni dereva mwenzake wa Mercedes kwenye Belgian Grand Prix na Jumapili kwenye Italian Grand Prix.

MJerumani huyo amesema kitendo alichokifanya sio kizuri lakini nini atasema Zaidi ya kuamini watamsamehe na kusahau.

Amesema hilo litakuwa jambo kubwa na anaomba radhi kwa kitendo chake cha hovyo.

Rosberg, ambaye alichukuliwa hatua za kinidhamu na Mercedes alipotezea sauti za kuzomewa na mashabiki ambazo alisema ni watu wa kutoka Uingereza.

Jumapili huko MONZA akakumbana na kuzomewa tena kwa mara nyingine alipokwenda kuchukua taji lake la nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.