Wednesday, September 17, 2014
Adrian apigwa stop kucheza Vikings kisa kumcharaza mtoto wake
MCHEZAJI wa timu ya Cricket ya Minnesota Vikings Adrian Peterson amepigwa stop kufanya shughuli zote ambazo zinahusiana na timu mpaka kesi yake ya ukatili kwa mtoto itakapomalizika.
Mchezaji huyo mwenye miaka 29 alikamatwa wiki iliyopita na kutolewa kwa dhamana lakini bado aliachwa kwenye mchezo wa Jumapili wa timu hiyo ya Vikings.
Peterson anakabiliwa na madai ya kumpiga mtoto wake na tawi la mti japo mwenyewe anasema alikuwa akimtia adabu na hakuwa na lengo la kumuumiza.
Tukio hilo limetokea mwezi May na mchezaji huyo akikutwa na hatia anaweza kufungwa jela miaka miwili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.