Monday, September 22, 2014

Ndumbaro aichambua mikataba ya soka

Bila shaka umeshasikia migogoro mingi ya kisheria katika Soka hasa pale mchezaji anapohama kutoka klabu moja kwenda nyingine, kocha anapotimulia au kung’atuka na mengine mengi.

Sintofahamu ya nani yuko sahihi kisheria katika uamuzi na taratibu alizozichukua imekuwa chanzo cha migogoro mingi na mabishano kati ya muhusika aliyechukua hatua hiyo na klabu husika. Wakati mwingine huzua zogo lisilokuwa na majibu kwa mashabiki na wadau wa soka nchini.

Kwa kutambua hilo, kipindi cha Wizara ya Michezo cha 100.5 Times Fm kinamkaribisha daktari wa sheria aliyebobea katika sheria Dr. Damas Ndumbaro ili kutoa ufafanuzi na elimu ya kisheria kuhusu matatizo hayo yanayoonekana kukithiri kwa sasa.

Msikilizaji anaalikwa kuuliza maswali yote ya sheria ya soka katika mikataba na Leo kuanzia saa moja kamili usiku, Dr Ndumbaro atayajibu hayo kitaalamu.

Unaweza kuuliza swali lako kupitia Ukurasa wa Facebook wa 100.5 Times Fm, ambao ni ‘Times Fm Tz’ au kutuma ujumbe mfupi wa simu wakati kipindi kitakapokuwa hewani.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.