Tuesday, September 9, 2014

Fabregas akiri mapenzi yake kwa Arsenal


Cesc Fabregas amekiri kuwa siku zote anajisikia kama mshika bunduki wa Arsenal lakini moyo wake wote kwasasa ameuweka Chelsea.

Fabregas alitua Stamford Bridge akitokea Barcelona kwa dau la paundi milioni 30 na mpaka sasa katika ligi ametoa pasi za kusaidia nne katika mechi tatu za ligi kuu.

Arsenal walikuwa na nafasi ya kumrejesha tena kiungo huyo kufuatia kipengele cha mkataba kilichokuwepo lakini wakaachana na mpango huo kabla ya Chelsea kutumbukia na kumnasa.

Anasema alikuwa anataka kurudi London akazungumza na wakala wake kumtafutia timu na ndipo ilipotua ofa ya Chelsea na akazungumza na Mourinho ambaye alimwambia mambo ambayo alikuwa anataka kuyasikia,akajisikia mwenye thamani na akajisikia kuwa sehemu ya kitu muhimu.

Anasema miaka mitano nyuma kama unamwambia kuhusu kucheza Chelsea na Mourinho asingeweza kuelewa lakini maisha yanabadilika.

Kiungo huyo mwenye miaka 27 anasema licha ya mapenzi aliyonayo kwa Arsenal lakini hana tatizo kucheza dhidi ya timu hiyo na jambo hilo aliliwaza kabla ya kusaini Chelsea na alifahamu anaposaini kwenye timu hiyo iko siku atarudi Emirates kucheza dhidi ya Arsenal jambo ambalo kwake anasema litakuwa la kipekee.

Ameongeza kuwa anakumbuka alicheza fainali dhidi ya Barcelona lakini anaapa kuwa alicheza kwa motyo wake wote na alitaka kushinda mchezo huo japo alikuwa akicheza dhidi ya timu iliyomlea tokea alipokuwa mdogo kitu ambacho pia kitatokea atakapocheza dhidi ya Arsenal akiwa na Chelsea.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.