Tuesday, September 30, 2014

MATOKEO MABOVU : Kocha wa Newcastle ajisalimisha kwa mmiliki

Meneja wa Newcastle Alan Pardew anatarajia kuwa na mazungumzo ya kina na mmiliki wa timu hiyo Mike Ashley baada ya kichapo cha jana cha bao 1-0 dhidi ya Stoke City.

Ashley alikuwepo kwenye uwanja wa Britannia akiitazama timu yake ikizamishwa kwa bao la Peter Crouch na kuiacha timu hiyo ikikamata nafasi ya pili kutoka mkiani.

Mashabiki wa klabu hiyo wameendelea kumbebea mabango wakitaka atimuliwe kazi.
 



Maujuzi ya Times Fm The Dream Team ndani ya Kisarawe

Mambo ya Kisarawe Times Fm The Dream Team vs Kisarawe Veterans mechi ambayo ilimalizika kwa The Dream Team kufungwa kwa taabu 1-0.

Nahodha wa Times Fm The Dream Team miye mwenyewe sasa...

Kikao cha dharura
Mkurugenzi wa Times Fm Rehure Nyaulawa akichanja mbuga

Monday, September 22, 2014

Ndumbaro aichambua mikataba ya soka

Bila shaka umeshasikia migogoro mingi ya kisheria katika Soka hasa pale mchezaji anapohama kutoka klabu moja kwenda nyingine, kocha anapotimulia au kung’atuka na mengine mengi.

Sintofahamu ya nani yuko sahihi kisheria katika uamuzi na taratibu alizozichukua imekuwa chanzo cha migogoro mingi na mabishano kati ya muhusika aliyechukua hatua hiyo na klabu husika. Wakati mwingine huzua zogo lisilokuwa na majibu kwa mashabiki na wadau wa soka nchini.

Kwa kutambua hilo, kipindi cha Wizara ya Michezo cha 100.5 Times Fm kinamkaribisha daktari wa sheria aliyebobea katika sheria Dr. Damas Ndumbaro ili kutoa ufafanuzi na elimu ya kisheria kuhusu matatizo hayo yanayoonekana kukithiri kwa sasa.

Msikilizaji anaalikwa kuuliza maswali yote ya sheria ya soka katika mikataba na Leo kuanzia saa moja kamili usiku, Dr Ndumbaro atayajibu hayo kitaalamu.

Unaweza kuuliza swali lako kupitia Ukurasa wa Facebook wa 100.5 Times Fm, ambao ni ‘Times Fm Tz’ au kutuma ujumbe mfupi wa simu wakati kipindi kitakapokuwa hewani.

FORMULA1 : Hamilton hawazi ubingwa kabisaaaa


DEREVA wa Mercedes Lewis Hamilton amesisitiza ubingwa wa dunia hauko akilini mwake licha ya kuongoza kwa mara ya kwanza ndani ya miezi minne.

Hamilton amesema hafikirii kuhusu ubingwa akisema bado anajihisi yupo mawindoni.

Azarenka nje msimu mzima


Victoria Azarenka atakosa sehemu ya msimu iliyobakia kwasababu ya kuumia mguu.

Bingwa huyo mara mbili wa Australian Open tayari amekosa miezi mitano ya mwaka huu 2014 na ameanguka mpaka nafasi ya 25 katika ubora wa viwango vya mchezo wa Tennis kwa wanawake kutokea nafasi ya pili.

Azarenka, 25,alifika kwenye hatua ya robo fainali ya US Open mapema mwezi huu na alikuwa arudi kwenye kwenye michuano ya Wuhan Open huko China.

Wednesday, September 17, 2014

Uefa Champions league leoooo....


Ligi ya mabingwa barani Ulaya inataraji kuendelea tena leo.

Mechi za leo

Adrian apigwa stop kucheza Vikings kisa kumcharaza mtoto wake


MCHEZAJI wa timu ya Cricket ya Minnesota Vikings Adrian Peterson amepigwa stop kufanya shughuli zote ambazo zinahusiana na timu mpaka kesi yake ya ukatili kwa mtoto itakapomalizika.

Mchezaji huyo mwenye miaka 29 alikamatwa wiki iliyopita na kutolewa kwa dhamana lakini bado aliachwa kwenye mchezo wa Jumapili wa timu hiyo ya Vikings.
Peterson anakabiliwa na madai ya kumpiga mtoto wake na tawi la mti japo mwenyewe anasema alikuwa akimtia adabu na hakuwa na lengo la kumuumiza.

Tukio hilo limetokea mwezi May na mchezaji huyo akikutwa na hatia anaweza kufungwa jela miaka miwili.