Monday, October 27, 2014
Nahodha timu ya Taifa auwa kwa kupigwa risasi,kisa ni kumtetea mpenzi
NAHODHA wa Bafana Bafana na Orlando Pirates Senzo Meyiwa ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa akijaribu kumtetea mpenzi wake kuporwa nyumbani kwake karibu na Johannesburg.
Golikipa huyo wa Orlando Pirates mwenye miaka 27 amefariki jana baada ya kupigwa risasi kifuani nyumbani kwa mpenzi wake Kelly Khumalo,ambaye ni muigizaji na muimbaji katika mji wa Vosloorus.
Watu wawili waliingia na kutaka kupewa simu za mkononi,pesa na vitu vingine vya thamani.
Afisa wa usalama katika mji huo Sizakele Nkosi-Malubane amesethibitisha tukio hilo na kusema kuwa Senzo alikuwa akimkinga mpenzi wake ambaye alikuwa amenyooshewa bunduki na mmoja wa watu hao.
Meyiwa alithibitika kufariki alipofikishwa hospitali.
Police nchini humo wamesema watu wawili waliingia katika nyumba hiyo saa 2 usiku wakati mwingine mmoja alikuwa akisubiri nje na wote watatu walikimbia baada ya tukio hilo.
Polisi wamesema kuwa watahakikisha wauaji hao wanakamatwa na tayari zawadi ya randi 150,000 imetangazwa kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji.
Meyiwa aliiongoza Africa Kusini Bafana bafana katika mechi zake nne zilizopita za kuisaka tiketi ya kucheza fainali za Africa mwakani bila kuruhusu goli na Jumamosi aliiongoza timu yake kusonga nusu fainali ya South African League Cup.
Wednesday, October 22, 2014
Chelsea majanga..
Jose Mourinho amekumbwa na uhaba wa washambuliaji kunako kikosi chake kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Manchester United utakaopigwa Jumapili.
Licha ya kukabiliwa na uhaba huo wa washambuliaji Mourinho amesema hana wasiwasi wowote na mchezo huo.
Chelsea tayari wapo bila ya Diego Costa aliyeukosa pia mchezo wa ligi ya mabingwa jana usiku dhidi ya Maribor mchezo ambao uliwafanya Chelsea kumpoteza Loic Remy aliyeumia katika dakika ya 16 baada ya kufunga bao la kuongoza.
Hiyo inamaanisha sasa Chelsea wanabakiwa na mshambuliaji Didier Drogba pekee ambaye naye hapo jana usiku alifunga bao lake la kwanza tokea amerejea katika timu hiyo.
Usiku wa rekodi Champions league,Mechi 8 goli 40
Shakhtar Donetsk wamepata ushindi wa rekodi ya ushindi mkubwa ugenini katika champions league wakiichapa Bate Borisov mabao 7-0 katika usiku ulioweka rekodi ya kufungwa mabao 40 kwa usiku mmoja.
Ni mabao mengi kufungwa katika usiku mmoja katika mechi nane ingawa imewahi kutokea kufungwa mabao 44 mwaka 1997 lakini ilihusisha mechi 12 kuchezwa katika usiku huo.
Shakhtar wamepata ushindi kama ambao waliwahi kuupata Olympic Marseille dhidi ya MSK Zilina mwaka 2010 huku mshambuliaji Luiz Adriano akifunga mabao matano akifikisha rekodi sawa na Lionel Messi kufunga idadi hiyo katika mchezo mmoja.
Katika mechi nyingine zilizochezwa jana usiku.
- CSKA 2 - 2 Man City FT
- Roma 1 - 7 Bayern Mun FT
- Apoel Nic 0 - 1 Paris St G FT
- Barcelona 3 - 1 Ajax FT
- Chelsea 6 - 0 NK Maribor FT
- Schalke 4 - 3 Sporting FT
- FC Porto 2 - 1 Ath Bilbao FT
Rekodi za ushindi mkubwa Champions
|
|
Result
|
Year
|
8-0 Liverpool FC v Besiktas
|
November 2007
|
7-0 Juventus v Olympiakos
|
December 2003
|
7-0 Arsenal FC v Slavia Prague
|
October 2007
|
0-7 MSK Zilina v Marseille
|
November 2010
|
7-0 Valencia v KRC Genk
|
November 2011
|
7-0 Bayern Munich v Basel
|
March 2012
|
0-7 Bate Borisov v Shakhtar Donetsk
|
October 2014
|
Wednesday, October 8, 2014
Mayweather sasa amtaka Pacquiao
KAMA ukisoma taarifa ya Jeff Mayweather kaka wa bondia Floyd Mayweather Jr ambayo ameituma inaonesha huenda likapigwa pambano ambalo limepachikwa jina la MEGA FIGHT kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao.
Huenda pambano hilo likafanyika mwakani wakati ambao Mayweather ameweka bayana kuwa ataachana rasmi kucheza mchezo huo.
Floyd Mayweather Sr yeye anathibitisha kuwa pambano hilo linaweza kuwepo lakini kama tu Pacquiao raia wa Filipino atashinda pambano lake dhidi ya Chris Algieri.
Mayweather Sr amesema katika pambano hilo anaamini kuwa mtoto wake atashinda kirahisi kama pambano hilo litafanyika.
Subscribe to:
Posts (Atom)