Friday, February 6, 2015

Mtoto wa miaka sita ampa ajira Mourinho Villa Park



KIJANA mdogo wa miaka sita mshabiki wa Aston Villa,Jude Branson amemuandikia barua kocha wa Chelsea Jose Mourinho akimuomba kuhamia huko Villa park ili kuinusuru timu hiyo na janga la kushuka daraja huku akimtaka kutua pamoja na mshambuliaji Diego Costa.

Branson,amemtaka kocha huyo kuwakomboa katika kipindi hiki kigumu wanachukutana nacho wakiwa chini ya kocha Paul Lambert.

Katika barua yake dogo huyo amueleza jinsi anavyomzimikia Mourinho akisema ndiye kocha wake kipenzi hivyo akimuomba kuichukua Aston Villa huku akimuomba kutua na Costa.

Aston Villa kesho watakutana uso kwa uso na Chelsea huko Villa Park huku ikiwa imecheza mechi nane bila ushindi na ikicheza kwa saa 10 na dakika 12 bila ya kufunga goli lolote.

Wednesday, February 4, 2015

Barcelona washtukia mchezo mchafu wa Real Madrid



RAIS wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amefichua kuwa mahasimu wao Real Madrid wamehusika na mchezo wa uhamisho wa Neymar kiasi cha kutakiwa kuwasilisha ushahidi.

Bartomeu anasema hakuna ujanja walioufanya kwenye usajili huo na siku zote watasimama katika ukweli kwakuwa uhamisho huo ulifanywa chini ya mwanasheria anayeheshimika.

Anasema kuna klabu nyingine zilimtaka Neymar na wakataka kulipa pesa nyingi Zaidi lakini wakashindwa na hilo hawakulipenda.

Ameongeza kuwa baba wa Neymar alimwambia kuwa Neymar kwa wakati huo alikuwa akiwaniwa na klabu mbili tu Barcelona na Real Madrid na wapinzani wao walikuwa tayari kutoa kitita kinene Zaidi.

Bartomeu pia amesema nyuma ya suala ya Neymar kuna kampeni za kisiasa dhidi ya klabu hiyo kuhusiana na kutaka kujitenga na kujitegemea kwa Catalunya.

Mendes asema Mourinho ndiye mrithi wa Ferguson



Super-agent Jorge Mendes amemwagia sifa mteja wake kocha Jose Mourinho akisema ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuchukua utawala wa Sir Alex Ferguson ambaye ameacha historia kubwa kwa timu ya Manchester United.

Ferguson,ambaye alishinda mataji 38 katika miaka 26 aliyokuwepo huko Old Trafford alistaafu mwaka 2013 na nafasi yake ikachukuliwa na David Moyes ambaye hata hivyo alidumu kwa miezi 10 pekee.

Mendes anasema ni ngumu kumpata mtu kama Ferguson kwasababu alikuwa ana akili ya ziada na kumtafuta mtu wa aina hiyo ni ngumu lakini akasema kwa England sasa wana mmoja tu ambaye ni Mourinho.

Anasema Mourinho kwasasa anaweza kufanya hilo kwa Chelsea kwasababu anawapenda mashabiki,anaupenda mji na anafikiri kuwa taka Zaidi ya miaka 10.