KIJANA mdogo wa miaka sita mshabiki wa Aston Villa,Jude
Branson amemuandikia barua kocha wa Chelsea Jose Mourinho akimuomba kuhamia
huko Villa park ili kuinusuru timu hiyo na janga la kushuka daraja huku
akimtaka kutua pamoja na mshambuliaji Diego Costa.
Branson,amemtaka kocha huyo kuwakomboa katika kipindi hiki
kigumu wanachukutana nacho wakiwa chini ya kocha Paul Lambert.
Katika barua yake dogo huyo amueleza jinsi anavyomzimikia
Mourinho akisema ndiye kocha wake kipenzi hivyo akimuomba kuichukua Aston Villa
huku akimuomba kutua na Costa.
Aston Villa kesho watakutana uso kwa uso na Chelsea huko Villa
Park huku ikiwa imecheza mechi nane bila ushindi na ikicheza kwa saa 10 na
dakika 12 bila ya kufunga goli lolote.